JINA LA CHAPA

Bio‑Oil®


JINA LA BIDHAA NA UKUBWA

Body Lotion 175ml
Body Lotion 250ml


ISHARA

Kwa kiasi kikubwa huongeza ulainishaji wa ngozi.


ONYESHO

Kioevu cheupe.


MUUNDO

Losheni yenye asilimia 42% ya viungo vya kuziba na asilimia 14% ya vitia unyevu.


VIUNGO

Aqua, Dimethicone, Isopropyl Palmitate, Ethylhexyl Cocoate, Isododecane, Isopropyl Myristate, Urea, Polyglyceryl-2 Dipolyhydroxystearate, Glycerin, Pentylene Glycol, Dicaprylyl Carbonate, Polyglyceryl-3 Diisostearate, Sodium Lactate, Dipentaerythrityl Hexacaprylate / Hexacaprate, Gluconolactone, Rosa Canina Fruit Oil, Simmondsia Chinensis Seed Oil, Calendula Officinalis Extract, Butyrospermum Parkii Oil, Helianthus Annuus Seed Oil, Glycine Soja Oil, Isostearyl Isostearate, Bisabolol, Octyldodecyl PCA, Retinyl Palmitate, Tocopheryl Acetate, Linoleic Acid, Linolenic Acid, Tocopherol, Sodium PCA, Sodium Hyaluronate, Lactic Acid, Stearalkonium Hectorite, Propylene Carbonate.


TATHMINI YA USALAMA

Bio‑Oil® Body Lotion imefanyiwa tathmini ya usalama na mtaalamu wa sumu aliyehitimu na imeainishwa kuwa salama kwa matumizi yake yaliyokusudiwa na watu wazima, ikiwa ni pamoja na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha, na watoto zaidi ya umri wa miaka mitatu.


JARIBIO LA KIMATIBABU LA NGOZI KAVU

Kituo cha majaribio Complife Italia S.r.l, Italia. Lengo Tathmini ya kimatibabu ya kupima ufanisi wa Bio‑Oil® Body Lotion katika kuboresha ulainishaji wa ngozi. Sampuli Wahusika: Washiriki 30 wa kike wenye afya nzuri walio na aina ya ngozi ya Fitzpatrick II-V na wanaonekana kuwa na ngozi kavu / kavu sana kuanzia sehemu ya chini ya nje ya miguu. Eneo la jaribio: bidhaa inayojaribiwa ilitumiwa kwenye sehemu ya nje ya mguu wa chini wa wahusika wote. Umri wa washiriki: 25–65. Mbinu Utafiti kifani unaodhibitiwa, wa sehemu tofauti za mwili, unaomficha mtathmini, na wa nasibu. Washiriki waliosha miguu yao kwa sabuni ili kusababisha ngozi kavu kwa kipindi cha siku 7. Tathmini msingi ya kimatibabu na ya kifani ilichukuliwa. Bio‑Oil® Body Lotion ilitumika mara mbili kila siku kwa siku 28 kwenye mguu wa sehemu ya chini, mguu huo mwingine ulibaki bila kutibiwa. Tathmini za kimatibabu na za kifani zilifanyika siku ya 1, 3, 6, 8, 10, 14, 21 na 28. Eneo lisilotibiwa lilitathminiwa pia nyakati zote. Wahusika walipewa alama za kimatibabu kulingana ukavu wa ngozi (kwenye mizani inayoanzia 0-5) na mtathmini mtaalamu wa kuangalia. Kipimo cha kiasi cha unyevu wa ngozi kilifanywa kwa kutumia Corneometer. Kipimo cha kiasi cha maji kinachotoka kwenye ngozi (TEWL) kama kiashiria cha kazi ya kuzuia, kilitoka Tewameter. Kwa kuongezea, dodoso la kujitathmini lilikamilishwa katika siku ya 8 na 14. Matokeo Ikilinganishwa na eneo lisilotibiwa, matibabu kwa kutumia Bio‑Oil® Body Lotion yalisababisha uboreshaji muhimu kitakwimu katika ualamishaji wa kiwango cha ukavu, vipimo vya Tewameter na Corneometer, kuanzia mapema kama siku ya 1, na nyakati zote. Kwa uanishaji wa kimatibabu wa kiwango cha ukavu, maboresho muhimu kitakwimu yalishuhudiwa katika asilimia 96.7% ya washiriki kutoka siku ya 14 na kuendelea, karibu mara mbili ya uboreshaji ulioonekana siku ya 1. Baada ya siku 28 za matumizi, asilimia 100% ya washiriki walionyesha ongezeko kubwa la unyevu wa ngozi, huku kiwango cha kupata nafuu kikiwa karibu mara 4 ya siku ya 1. Vivyo hivyo, baada ya siku 28 za matumizi, asilimia 100% ya washiriki walionyesha kupungua pakubwa kwa TEWL, huku kiwango cha kupata nafuu kikizidi mara mbili ya siku ya 1. Matokeo haya yanaungwa mkono na matokeo ya dodoso la kujitathmini.


JARIBIO LA MTUMIAJI MWENYE NGOZI KAVU

Kituo cha majaribio Utafiti wa Kimataifa wa Ayton, Uingereza. Lengo Kutathmini utendaji wa Bio‑Oil® Body Lotion kama mafuta ya kulainisha ngozi. Sampuli Wahusika: Washiriki 119 wa kike walio katika hali nzuri ya afya. Umri wa washiriki: 25–65. Mbinu Jaribio la mtumiaji la wiki 2, la kutumika mara moja nyumbani. Washiriki waliagizwa kutumia bidhaa mara mbili kila siku, asubuhi na jioni. Singa kwenye ngozi hadi ifyonzwe kabisa. Maswali matatu mafupi yalikamilishwa: la kwanza baada ya bidhaa kutumiwa kwa mara ya kwanza, la pili baada ya saa 12, na la tatu baada ya wiki 2 za kutumia bidhaa. Matokeo Matumizi: Asilimia 95% ya washiriki walikubali kwamba ''bidhaa hii ni nyepesi kuliko kilainisha ngozi chochote ambacho wamekitumia hapo awali''. Asilimia 93% ya washiriki walikubali kwamba ''bidhaa hii inaenea kwa urahisi zaidi kuliko kilainisha ngozi chochote ambacho wamekitumia hapo awali''. ufyonzaji: Asilimia 82% ya washiriki walikubali kwamba ''bidhaa hii inafyonzwa kwa urahisi zaidi kuliko kilainisha ngozi chochote ambacho wamekitumia hapo awali''. Asilimia 75% ya washiriki walikubali kwamba ''bidhaa hii inafyonzwa kwa haraka zaidi kuliko kilainisha ngozi chochote ambacho wamekitumia hapo awali''. Asilimia 74% ya washiriki walikubali kwamba ''bidhaa hii haiachi mabaki ya mafuta baada ya kutumika''. Asilimia 86% ya washiriki walikubali wamba ''baada ya kutumia bidhaa hii waliweza kuvaa nguo mara moja''. Unyevu: Asilimia 93% ya washiriki walikubali kwamba ''bidhaa hii huacha ngozi ikihisi ikiwa na unyevu mara moja''. Asilimia 92% ya washiriki walikubali kwamba ''baada ya kutumia bidhaa hii ngozi yao ilihisi laini na nyororo''. Asilimia 90% ya washiriki walikubali kwamba ''ngozi yao ilihisi kuwa ina unyevu siku nzima'' na asilimi 91% walikubalia kuwa ''ngozi yao inahisi laini na nyororo siku nzima''. Asilimia 92% ya washiriki walikubali kwamba ''ngozi yao inaonekana bora zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzoni mwa kipindi cha wiki ya 2''. Kwa ujumla: Asilimia 73% ya washiriki walikubali kwamba ''bidhaa hii ni bora zaidi kuliko kilainisha ngozi chochote ambacho wamekitumia hapo awali''.


JARIBIO KWENYE NGOZI INAYOATHIRIKA KWA URAHISI

Kituo cha majaribio Complife Italia S.r.l, Italia. Lengo Kutathmini uwezo wa Bio‑Oil® Body Lotion kusababisha Mwasho wa ngozi. Sampuli Wahusika: Washiriki 25; 3 wa kiume na 22 wa kike, wote wakiwa na ngozi inayoathirika kwa urahisi kulingana na jaribio la kuathiriwa na asidi ya maziwa. Umri wa washiriki: 18–70. Mbinu Utafiti unaodhibitiwa. Maeneo mawili yalitathminiwa: eneo ambalo udhibiti hasi ulitumika (maji yaliyosafishwa) na eneo ambalo Bio‑Oil® Body Lotion ilitumika. Bidhaa zinazojaribiwa zilitumiwa kwenye migongo ya washiriki, kwenye ngozi, kwa kipindi cha saa 48 kwa kutumia Finn Chamber®. Matokeo ya ngozi yalitathminiwa chini ya usimamizi wa daktari wa ngozi, ili kutathmini mwasho wa kwanza wa ngozi kwa dakika 15, saa 1 na saa 24 baada ya kuondolewa kwa pamba. Matokeo ya ngozi yalikadiriwa kwenye mizani inayoanzia 0-4 (huku 0 ikiwa hakuna harara, uvimbe, au aina nyingine za mwasho wa ngozi, na 4 ikiwa harara na uvimbe mkali, inayoashiria mwonekano wa rangi nyekundu iliyokolea na uvimbe ulioenea zaidi ya eneo lililotumika). Matokeo Uwezo wa ngozi kustahimili Bio‑Oil® Body Lotion ulichukuliwa kuwa ''usiowasha''.


JARIBIO LA KUTOSABABISHA CHUNUSI

Kituo cha majaribio Complife Italia S.r.l, Italia. Lengo Kutathmini uwezo wa Bio‑Oil® Body Lotion kusababisha chunusi. Sampuli Wahusika: Washiriki 20; 14 wa kike na 6 wa kiume kutoka makabila tofauti wenye ngozi inayothiriwa na chunusi. Umri wa washiriki: 18–65. Mbinu Utafiti unaodhibitiwa. Bidhaa hiyo ilitumiwa kwenye karatasi ya ufyonzaji na kupakwa kwenye eneo la juu la migongo ya washiriki. Pamba hizo ziliachwa kwa saa 48 hadi 72, zikaondolewa na kutumiwa tena. Jumla ya pamba 12 zilitumika kwa wiki 4 mfululizo. Maeneo matatu yalitathminiwa kwa kulinganisha udhibiti hasi (maji yaliyosafishwa), bidhaa inayojaribiwa (Bio‑Oil® Body Lotion) na udhibiti chanya (kileo cha lanolin, bidhaa inayojulikana kusababisha chunusi). Matokeo ya ngozi yatathminiwa chini ya usimamizi wa daktari wa ngozi dakika 15 baada ya kuondolewa kwa kila pamba ili kulinganisha uwepo wa mabaka kabla na baada ya kutumiwa kwa kila bidhaa. Matokeo Bio‑Oil® Body Lotion ilipatikana kuwa haisababishi chunusi. Eneo ambalo Bio‑Oil® Body Lotion ilitumika halikuonyesha tofauti kubwa ikilinganishwa na eneo la udhibiti hasi. Udhibiti chanya ulisababisha chunusi.


UTAFITI WA UNATO

Kituo cha majaribio Union Swiss, Afrika Kusini. Lengo Utafiti wa ndani wa kutathmini nguvu ya unato wa Bio‑Oil® Body Lotion ikilinganishwa na bidhaa sawia za kulainisha ngozi. Sampuli Kulinganisha Bio‑Oil® Body Lotion na bidhaa 13 za kulainisha ngozi zilizotengenezwa na makampuni 10 ya kimataifa yenye historia thabiti katika ulainishaji wa ngozi. Mbinu Nguvu ya unato ilisomwa kwa kutumia Anton Paar RheoLab QC rheometer, kwa kutumia spindle CC 39, kasi: 200 rpm kwa 20C, kiwango cha ulaini: 155. Matokeo Bio‑Oil® Body Lotion ilipatikana kuwa na nguvu ya chini mara 7.5 ya unato ikilinganishwa na wastani wa bidhaa za washindani (94 mPa.s vs. 707 mPa.s mtawalia), inayoashiria uowevu mwembamba, mwepesi ambao ni rahisi na haraka zaidi kufyonzwa.


MATUMIZI

Jinsi ya kutumia Bio‑Oil® Body Lotion inapaswa kusingwa kwa mwendo wa mviringo kwenye mwili hadi ifyonzwe kabisa. Inashauriwa kwamba Bio‑Oil® Body Lotion itumike mara mbili kila siku, asubuhi na jioni. Bio‑Oil® Body Lotion haipaswi kutumiwa kwenye kidonda wazi au ngozi iliyokatika. Imekusudiwa kutumiwa kama kipodozi tu. Tikisa kabla ya kutumia Bio‑Oil® Body Lotion ni emalshani ambayo maji na mafuta yamunganishwa pamoja kwa urahisi sana. Kwa urahisi sana, hadi wakati yameachwa yametulia baadhi ya mafuta hupanda juu ya bidhaa na kuunda safu nyembamba. Kwa kutikisa bidhaa hiyo polepole kabla ya matumizi, safu ya mafuta hutawanyika tena kwenye losheni. Uundaji wa tabaka unaweza kuchukua siku kadhaa kuanzia siku tatu hadi wiki tatu na unategemea sababu kama vile halijoto, jinsi chupa inavyotikiswa kwa nguvu na mara ngapi imetikiswa. Kitendo cha kutumia bidhaa hii kila siku, kugeuza chupa juu chini wakati wa kuitumia, imetosha kuhakikisha kuwa safu hii ya mafuta haitokei. Ikiwa safu ya mafuta imeundwa na bidhaa hiyo itumike bila kutikiswa, mchanganyiko wazi wa mafuta unaweza kutiririka kutoka kwenye chupa. Hii si hatari kwa usalama wa watumiaji. Muda wa kutumia Jaribio la kimatibabu la Bio‑Oil® Body Lotion limefanywa kwa kipindi cha wiki nne, hivyo kuruhusu utendaji wa bidhaa hiyo kutathminiwa baada ya muda. Uchambuzi wa takwimu unaonyesha uboreshaji mkubwa katika mwonekano wa ngozi baada ya saa 24 na kwamba uboreshaji huu unadumishwa kwa muda wa jaribio lote. Hata hivyo Bio‑Oil® Body Lotion inaweza kutumika kila wakati kwa ajili ya sifa zake za kulainisha na kuboresha ngozi, hivyo kuifanya kuwa sehemu ya utaratibu wa kila siku wa ngozi. Tumia pamoja na utaratibu wa utunzaji wa ngozi Kwa ufyonzaji wa juu zaidi, Bio‑Oil® Body Lotion inapaswa kutumiwa kwenye ngozi iliyosafishwa baada ya kuoga. Ikiwa unatumia losheni ya kukinga jua au krimu nyingine fanya hivyo tu baada ya Bio‑Oil® Body Lotion kufyonzwa kabisa kwenye ngozi. Kutumia wakati wa ujauzito Bio‑Oil® Body Lotion ni salama kutumia wakati wa ujauzito. Vitamini A na ujauzito Wanawake kwa kawaida wanapendekezewa kupunguza virutubisho vya vitamini A wakati wa ujauzito na kwa hivyo wanaweza kuwa na wasiwasi kuhusu kutumia bidhaa za ngozi zenye vitamini A. Dutu yoyote inayotumika kwenye ngozi ni hatari tu ikiwa iko katika viwango vya juu kuliko kiwango chake cha juu cha sumu. Kwa sababu ngozi hutoa kizuizi kikubwa cha upenyaji, sehemu ndogo tu ya vitamini A inayotumiwa ndio huingia mwilini. Kamati ya Sayansi ya Tume ya Ulaya kuhusu Usalama wa Watumiaji (SCCS) imetathmini vitamini A na michanganyiko yake, inapotumiwa kama viungo vya vipodozi. Maoni ya SCCS ni kwamba matumizi ya vitamini A katika losheni za mwili, hadi kiwango cha juu zaidi cha asilimia 0.05% ya retinoli, ni salama. Vitamini A iliyopo katika muundo wa Bio‑Oil® Body Lotion iko chini ya kiwango hiki cha juu zaidi kinachoruhusiwa kwa losheni ya mwili na inaweza kutumika kwa usalama wakati wa ujauzito. Kutumia wakati wa kunyonyesha Bio‑Oil® Body Lotion ni salama kutumiwa kwenye mwili wakati wa kunyonyesha, lakini inapendekezwa kuepuka kutumia kwenye chuchu. Ingawa hakuna madhara yanayoweza kutokea, watoto wachanga wanaweza kuathiriwa kwa urahisi na hawapaswi kumeza Bio‑Oil® Body Lotion, hata kwa kiasi kidogo sana. Matumizi kwa watoto wachanga na wakubwa Usalama wa kutumia Bio‑Oil® Body Lotion kwa watoto chini ya umri wa miaka mitatu haujatathminiwa. Katika miaka michache ya kwanza baada ya kuzaliwa, mabadiliko mengi hufanyika katika mwili wa binadamu, ikiwa ni pamoja na kukua kwa mfumo wa kinga. Kwa hivyo inashauriwa kwamba itumiwe tu kwa watoto wenye umri wa miaka mitatu au zaidi. Kutumia kwenye jua Majaribio yaliyofanywa kwenye Bio‑Oil® Body Lotion yalionyesha kuwa bidhaa hii haiwezeshi au kuzidisha kuchomwa na jua. Kwa hivyo ni salama kutumia kwenye jua, hata hivyo bidhaa hii haitoi kinga dhidi ya madhara ya mionzi ya jua ya UVA na UVB na hivyo ni muhimu kutumia bidhaa hii pamoja na bidhaa nyingine za kukinga mionzi ya jua zenye sifa ya kukinga jua (SPF) ya angalau 30. Kutumia kwenye au karibu na tando telezi Bio‑Oil® Body Lotion imeainishwa kuwa salama kwa matumizi yote, hata hivyo usalama wake haujajaribiwa kwenye tando telezi kwani hii si sababu ya kutumia bidhaa hii. Kutumia pamoja na tibaredio au tibakemikali Ingawa Bio‑Oil® Body Lotion haina viungo vyovyote ambavyo vinaweza kufyonza mionzi, ni vyema kwa watu wanaopata tiba ya tibaredio au tibakemikali kutafuta ushauri wa daktari kabla ya kutumia bidhaa hii. Kutumia pamoja na bidhaa za dawa Bio‑Oil® Body Lotion ni bidhaa ya vipodozi. Kwa ushauri kuhusu kutumia bidhaa hii pamoja na kutumia bidhaa za dawa kwa wakati mmoja, ni bora kutafuta ushauri wa daktari. Kutumia kwenye ngozi inayoathirika kwa urahisi Bio‑Oil® Body Lotion inaweza kutumika kwenye ngozi inayoathirika kwa urahisi. Katika utafiti wa mwasho wa ngozi uliofanyiwa washiriki 25 wenye umri wa miaka 18-70 walio na ngozi inayoathirika kwa urahisi, hakuna wahusika waliopata madhara yoyote mabaya kutokana na muundo huu. Kuumia kwenye ngozi yenye mafuta Bio‑Oil® Body Lotion inaweza kutumiwa kwenye ngozi yenye mafuta. Katika jaribio lililofanyiwa washiriki 20 wenye umri wa miaka 18-65 wenye ngozi inayoathiriwa na chunusi, Bio‑Oil® Body Lotion ilipatikana kuwa haisababishi chunusi. Kutumia kwenye ngozi inayoathiriwa na chunusi Bio‑Oil® Body Lotion inaweza kutumiwa kwenye ngozi inayoathiriwa na chunusi. Katika jaribio lililofanyiwa washiriki 20 wenye umri wa miaka 18-65 wenye ngozi inayoathiriwa na chunusi, Bio‑Oil® Body Lotion ilipatikana kuwa haisababishi chunusi. Inashauriwa kwa watu wanaosumbuliwa na chunusi kutafuta ushauri wa daktari kabla ya kutumia Bio‑Oil® Body Lotion.


DALILI ZA NGOZI KAVU NA SABABU

Dalili Dalili za ngozi kavu ni pamoja na ngozi isiyopendeza na yenye madoa, mistari nyembamba, ngozi ya kijivu au yenye rangi ya kijivu na hisia ya kuparara na kubana. Sababu Ngozi kavu husababishwa na sababu za nje na za ndani. Sababu za nje: Hali ya hewa kavu husababisha unyevu kutolewa ndani ya ngozi, kupitia tabaka mbili za lipidi na kwenda kwenye hewa kavu nje. Viyoyozi na vipashaji joto huvuta unyevu nje ya hewa, na kuunda hali ya hewa kavu ambayo huvuta unyevu nje ya ngozi. Kuosha kila siku na kutumia sabuni kali husababisha tabaka mbili za lipidi za ngozi kuondolewa, na kuifanya iwe rahisi kwa unyevu kutoka kwenye ngozi. Sababu za ndani: Mwili unavyoendelea kuzeeka, ngozi hutoa lipidi chache hivyo kusababisha tabaka mbili za lipidi kuwa nyembamba na kuifanya iwe rahisi kwa unyevu kuondoka. Jenetiki zinaweza kuhusika katika kusababisha ngozi kavu kutokana na viwango vya chini vinavyotokea kwa kawaida vya keramidi katika tabaka mbili za lipidi. Hii inasababisha kupungua kwa uwezo wa kuziba wa kizuizi cha ngozi, na kuchangia viwango vya juu kuliko kawaida vya kupoteza unyevu. pH ya ngozi huathiri kazi ya kuzuia. Kiwango cha juu cha pH katika ngozi huharibu utendaji mzuri wa tabaka mbili za lipidi.


UTENGENEZAJI

Utengenezaji wa Bio‑Oil® Body Lotion unafuata mahitaji ya Kanuni Bora za Utengenezaji (GMP) ya ISO 22716: 2007 kwa bidhaa za vipodozi. Malighafi zote zinazotumika katika utengenezaji wa Bio‑Oil® Body Lotion zinaambatana na Cheti cha Uchanganuzi (COA), na vifaa vyote vya ufungaji vinaambatana na Cheti cha Ukubalifu (COC). Hakuna malighafi au vifaa vya ufungaji hutolewa ili kutengenezwa hadi vipite vipimo vya kudhibiti ubora. Kila bechi ya Bio‑Oil® Body Lotion iliyochanganywa imetengewa nambari ya kipekee ya bechi. Sampuli kutoka kwenye bechi hiyo hujaribiwa kwenye maabara ili kuangalia mwonekano, uwazi, harufu, utambulisho kwa kutumia na spectrophotometry, uzito, unato na mikrobiolojia. Sampuli huhifadhiwa kwa miaka minne. Ujazaji na ufungaji wa Bio‑Oil® Body Lotion hufanyika katika kituo kilichodhibitiwa halijoto na unyevu. Hewa hupita kupitia mfumo wa hali ya juu wa kuchuja hewa (HEPA) ili kuzuia uchafuzi wa vumbi. Wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye viwanda vya uzalishaji huvaa kofia, barakoa, ngao za uso, glavu, kanzu na vifuniko vya viatu. Sampuli huondolewa viwandani katika vipindi vya mara kwa mara na hukaguliwa na idara ya Udhibiti wa Ubora kama tahadhari dhidi ya kasoro isiyo ya kawaida. Nambari ya bechi huchapishwa kwenye chupa, katoni na shehena, na sampuli ya kubakiza kutoka kwenye kila bechi iliyotengenezwa huhifadhiwa kwa miaka minne. Hakuna uzalishaji hatari, taka hatari au maji machafu yanayotokana na uzalishaji wa Bio‑Oil® Body Lotion.


MAELEKEZO YA UHIFADHI

Bio‑Oil® Body Lotion inapaswa kuhifadhiwa mahali baridi, mbali na miali ya moja kwa moja ya jua.


UREJELEZAJI

Bidhaa zote zinazofunga Bio‑Oil® Body Lotion (chupa, kifuniko na katoni) zinaweza kutumiwa tena.


KIPINDI CHA BAADA YA KUFUNGUA (PAO)

Bio‑Oil® Body Lotion ina PAO ya miezi 12. Hii ni kipindi cha muda baada ya kufungua ambacho bidhaa ni salama na inaweza kutumika bila madhara yoyote kwa mtumiaji.


UTHIBITISHO

Bio‑Oil® Body Lotion imethibitishwa kuwa Halaal na Kosher.


MADHARA MABAYA

Ijapokuwa Bio‑Oil® Body Lotion ina maelezo salama yanayohusu sumu na inakidhi kanuni za kimataifa kuhusu suala hili, kama ilivyo katika bidhaa zote za vipodozi, kuna hatari kwamba watumiaji wa Bio‑Oil®® Body Lotion wanaweza kukumbana na madhara mabaya wakati wa kutumia bidhaa. Ikiwa madhara yoyote mabaya yatatokea, matumizi ya bidhaa yanapaswa kukomeshwa mara moja. Dalili za madhara mabaya ya ngozi zinaweza kujumuisha upele, na uvimbe, ambayo kwa kawaida hutokea katika eneo ambalo bidhaa hiyo ilitumika. Madhara haya yanaweza kuambatana na mwasho na usumbufu kidogo. Katika hali nyingi, madhara mabaya yatapungua ndani ya siku mbili hadi tatu baada ya matumizi ya bidhaa hiyo kukomeshwa. Hadi ngozi irudi hali yake ya awali, inaweza kuonekana kavu na iliyo parara madhara yakiendelea kupungua. Ikiwa una wasiwasi wowote kuhusu athari ya mzio inayoweza kutokea kutokana na kutumia Bio‑Oil® Body Lotion, ni busara kufanya jaribio rahisi la mzio ili kuangalia hii. Hii inafanywa kwa kutumia kiasi kidogo cha Bio‑Oil® Body Lotion kwenye kigasha cha ndani na kusubiri kwa muda wa saa 24 ili kuona ikiwa athari yoyote itatokea. Uwekundu unaoonekana wa ngozi (harara) au uvimbe mdogo wa ngozi (uvimbe) unaweza kuonyesha uwezekano wa athari ya mzio.


HAIJAJARIBIWA KWENYE WANYAMA

Bio‑Oil® Body Lotion na malighafi zake hutengenezwa viwandani kwa kufuata kanuni za EU zinazohusiana na kuwajaribu wanyama kwa madhumuni ya vipodozi. Bio‑Oil® Body Lotion, au viungo vyake vyovyote, havijajaribiwa kwenye wanyama na Bio‑Oil® au watoaji wao wowote wa malighafi.


HAINA BIDHAA ZA WANYAMA

Bio‑Oil® Body Lotion haina viungo vyovyote vinavyotokana na wanyama.


KUMEZA KWA BAHATI MBAYA

Katika tukio la kumeza kwa bahati mbaya Bio‑Oil® Body Lotion, haiwezekani kwamba athari yoyote mbaya zaidi ya hisia za kichefuchefu na kuhara zitapatikana kwa sababu Bio‑Oil® Body Lotion haina sumu. Hata hivyo, inashauriwa kutafuta ushauri wa matibabu, hasa katika hali ya mtoto mchanga au mkubwa kumeza kwa bahati mbaya.


MABADILIKO KATIKA MWONEKANO

Bio‑Oil® Body Lotion ina vitu vilivyotolewa kwenye kalendula na mafuta muhimu, pamoja na vitamini A palmitate, ambayo zote zinaathiriwa na jua. Kuwekwa kwenye jua kunaweza kusababisha mabadiliko ya rangi baada ya muda. Bio‑Oil® Body Lotion inapaswa kuhifadhiwa mbali na miali ya moja kwa moja ya jua.


TAREHE YA MWISHO KUSASISHWA

22 Agosti 2023