Sera ya faragha
Ili kuonyesha tovuti hii vizuri kwenye kifaa chako tunatumia maelezo ya kivinjari chako. Ikiwa tu utakubali matumizi yetu ya kuki, ndipo tutaweka faili ndogo za data kwenye kifaa chako ambazo hutuwezesha kukumbuka eneo, hatua na mapendeleo yako ili tuweze kuboresha uzoefu wako wa mtumiaji. Kando na matumizi yaliyo hapa juu, hatutashiriki data yako na wahusika wengine, isipokuwa iwe inahitajika na sheria.
Bio‑Oil® / Bi-Oil® / Bioil®
Bio‑Oil hutafiti na kuendeleza bidhaa maalum za utunzaji wa ngozi, kwa kutumia mafuta ili kufanikisha utendaji bora wa bidhaa. Nembo inajulikana kama Bio‑Oil® nchi zote isipokuwa Austria, Jamhuri ya Cheki, Ufaransa, Ujerumani, Slovakia na Uswisi ambapo jina la Bi-Oil® linatumika na nchini Japani jina la Bioil® linatumika.
Kuhusu
Mnamo 1987 Bio‑Oil ilitanguliza kutumia mafuta kusaidia kuboresha mwonekano wa kovu na alama za kunyoosha ngozi. Wakati huo karibu kila bidhaa kwenye rafu ilikuwa krimu au losheni, na bidhaa hii ilikabiliwa sana na nadharia ya kushuku. Leo bidhaa hii ni bidhaa ya kovu na alama ya kunyoosha ngozi inayoongoza dunia. Mnamo 2010 Bio‑Oil ilianzisha maabara maalum yenye msimamo wa kutafiti jinsi ya kutumia mafuta kutibu mashaka mengine ya ngozi. Mwaka wa 2018 jeli ya mafuta ya ngozi kavu ilizinduliwa na katika mwaka wa 2020 bidhaa ya kuondoa kovu na kulainisha ngozi iliyotengenezwa kutoka kwa mafuta asili asilimia 100 ilizinduliwa. Mwaka wa 2021 losheni yenye mafuta mengi ililetwa kwenye soko. Bio‑Oil huzingatia utafiti pekee, pamoja na kuuza na kusambaza bidhaa zake zenye leseni kwa kampuni za utunzaji wa ngozi dunia nzima. Kupata taarifa kuhusu bidhaa za Bio‑Oil, tafadhali tembelea duka lako la dawa.
Makovu na alama za kunyoosha ngozi
Mafuta yana uwezo wa ajabu kuboresha ngozi. Vipi na kwa nini, hayaeleweki kikamilifu kwa sababu faida ya mafuta inajulikana zaidi kama hadithi za kale tu. Bio‑Oil® Skincare Oil yalikuwa mafuta ya kwanza kuwasilishwa katika jaribio la kitabibu na kuthibitisha kwamba yanaweza kuboresha mwonekano wa makovu na alama za kunyoosha ngozi. Mafanikio ya majaribio haya yalichochea madaktari na wafamasia kote duniani kuanza kushauri matumizi ya bidhaa hii. Leo Bio‑Oil® Skincare Oil ni bidhaa ya kovu na alama ya kunyoosha ngozi inayoongoza duniani pamoja na kushinda zaidi ya tuzo 400 za utunzaji wa ngozi. Maelezo ya Bidhaa
Ngozi kavu
Njia bora ya kutatua ngozi kavu ni safu inayoziba kwenye ngozi ambayo inakomesha unyevu kukwepa. Bidhaa za kawaida kwa ngozi kavu (krimu, losheni na siagi) zina wastani wa asilimia 20 ya mafuta, nta au siagi kwa kusudi hili. Bio‑Oil® Dry Skin Gel inayo asilimia 84. Bio‑Oil® Dry Skin Gel ilianza kusambazwa kimataifa mwaka wa 2018. Maelezo ya Bidhaa
Makovu na alama za kunyoosha ngozi (uundaji wa asili)
Huku uhitaji wa bidhaa zilizotengenezwa kutoka kwa viungo vya asili ikiongezeka, Bio‑Oil imetengeneza bidhaa ya kovu na alama za kunyoosha ngozi kwa kutumia mafuta ya asili pekee. Matokeo ya majaribio ya kitabibu yalionyesha bidhaa hii kuwa nzuri kama bidhaa ya asili ya Bio‑Oil ya kovu na alama za kunyoosha ngozi, hivyo kufanya kuwa mara ya kwanza bidhaa ya asili imethibitishwa kulingana na utendakazi wa bidhaa inayoongoza katika kategoria. Bio‑Oil® Skincare Oil (Natural) ilianza usambazaji wake wa kimataifa katika mwaka wa 2020. Maelezo ya Bidhaa
Kuongezea unyevu wa mwili
Bidhaa bora inayoongeza unyevu lazima ifyonzwe mara moja na haiachi mabaki ya kuteleza, ili uweze kuvaa nguo papo hapo. Kwa kiufundi zaidi hii ni ngumu sana kwa sababu kuongeza unyevu kunahitaji kuacha safu ya mafuta kwenye ngozi ili kusaidia kushika vizuri unyevu wa ngozi ndani yake. Bio‑Oil® Body Lotion imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya utangulizi ya Bio‑Oil ya tikisa-kabla ya kutumia ambayo inaruhusu losheni kuwa na mafuta mengi na mwanga mwingi. Bio‑Oil® Body Lotion ilianzisha uzinduzi wake wa kimataifa mwaka wa 2021. Maelezo ya Bidhaa